Ouverture du I Centenaire de la mort du bienheureux MANUEL DOMINGO Y SOL

FONDATEUR DE LA FRATERNITÉ DE PRÊTRES OPÉRAIRES DIOCÉSAINS

 

ENTRÉE

1. Milango zetu zimefunguliwa tuingie sasa nyumbani mwa Bwana ; magombezi yote tuache nje, ni wakati sasa wa kusali.

Alleluia (bis)

Wamama na wamana na wazee na watoto, ingieni sasa nyumbani mwake Bwana Mungu wetu. Imbieni furaha (x 3)

2. Ref: Tuingie nyumbani mwa Bwana, tuingie nyumbani mwake

Karibu, ndugu, tuingie nyumbani mwake, tuingie.

Milango zetu zimefunguliwa tuingie sasa nyumbani mwa Bwana; magombezi yote tuache nje, ni wakati sasa wa kusali.

3. Ref: Nous marchons vers le Dieu Puissant en lui chantant un cantique nouveau et dans son sanctuaire il entend nos voix.

Marchons joyeusement jusqu’à son autel.

NAMWUNGAMIA

Namwungamia Mungu Baba (Ooh mimi) namwungamia Baba Mwenyezi (2x) nanyi ndugu zangu, ya kama nimefanya zambi tele, naungama. (2x)

Ooh mimi, naungama, ooh mimi naungama, Ooh mimi naungama zambi zangu. (2x)

Mawazo yangu yote, maneno yangu yote, matendo yangu naungama, (2x) na kwa kuacha mapashwa, mapashwa yangu yote, ndiyo kosa langu kubwa. (2x) Ndiyo maana naomba mama Maria, bikira mtakatifu situ zote. (2x), na malaika wote, na watakatifu wote, kuniombea kwa Bwana Mungu. (2x)

KYRIE

Bwana, utuhurumie. Kristu, utuhurumie. Bwana, utuhurumie.

SIFA

GLORIA: SFA KWA MUNGU

Ref: Sifa kwa Mungu juu mbinguni: twimbe sifa. Amani, amani duniani : twimbe sifa Kwa watu anaowapenda : tuimbe sifa.

  1. Tunakusifu, tunakuheshimu, Tunakuabudu, tunakutukuza, tunakushangilia kwa ajili ya sifa yako mkuu.

  2. Bwana Mungu, Mfalme wa mbingu, Mungu Baba Mwenyezi. Bwana Yesu Kristu. Mwana-kondoo wa Mungu Baba.

  3. Unayeondoa zambi za dunia, utuhurumie, utuhurumie. Unayeondoa zambi za dunia, upokee ombi letu. Unayekaa kuume kwa Baba, utuhurumie, utuhurumie.

  4. Kwa maana, TWIMBE SIFA wewe peke, peke yako, Mtakatifu. Pamoja naye Roho, naye Roho, Mtakatifu. Katika sifa yake, sifa yaske, Mungu Baba.

PSAUME

R. Tu n’as voulu ni sacrifice, Tu n’as voulu ni holocauste, mais tu m’as formé un corps.Alors j’ai dit : me voici, Me voici, Seigneur, je viens, Je viens pour faire ta volonté (bis)

  1. La voix du Seigneur disait : « Qui enverrai-je ? Qui ira pour nous ? » Je répondis : « Me voici, Seigneur ; me voici, Seigneur, envoie-moi. »

  2. La voix du Seigneur disait : « Bien avant ta naissance, je t’avais connu et consacré. Tu seras mon témoin. Tu seras mon témoin parmi les nations.

ACCLAMATION

Mimi mtumishi Bwana asema, ee Bwana, alleluia (2x)

Najua kondoo zangu, nao wanijua, alleluia.

OFFERTOIRE
  1. Mkate wetu twakutolea, Baba, Sadaka ya waana wako. Baba pokea pokea, Baba, pokea, Mwana, pokea, Mweo, sadaka ya waana wako.

  2. Ref: Ee, Baba, twaleta zawadi zetu

  1. Mkate na divai, ee Baba: twaomba uzipokee. Ni mazao ya mashamba, ee Baba: twaomba uzipokee.

  2. Tunaleta feza zetu, ee Baba: twaomba uzipokee. Ni mazao ya mashamba, ee Baba: twaomba uzipokee.

  3. Tunaleta furaha zetu, ee Baba: twaomba uzipokee. Ni alama la mapendo, ee Baba: twaomba uzipokee.

3. Ref: Nakuja, nakuja kutolea sadaka, ee mmi Nakuja, ee mimi, kutolea ee mimi, sadaka yangu: Uipokee!

Mwumba wa vyote, pokea, ee (2x) sadaka yangu, Bwana, pokea, ee Twakutolea, Bwana, pokea. Ni waana wako, Bwana, pokea, ee twakutolea sadaka yetu, Bwana pokea,ee (2x). Ee mimi, nakuja, ee mimi, kutolea mimi sadaka yangu, uipokee.

MTAKATIFU

Mtakatifu (x4) Bwana Mungu wa ulimwengu Mbingu na dunia zimejaa sifa yako, oo Hosanna!

Réf. Hosanna! (x4)

    1. Tuimbe wote, ee. Hosanna! Mtoto wa Daudi.Hosanna! Ni Mungu wetu, uu. Hosanna! tumsifu milele, ee. Hosanna! milele na milele, ee. Hosanna!
    2. Mbarikiwa yule anayekuja kwa jina la Bwana, aa. Hosanna !

AGNUS DEI

Agneau de Dieu qui enlèves le péché du monde, prends pitié de nous (2x).

Agneau de Dieu qui enlèves le péché du monde, prends pitié de nous (2x).

Agneau de Dieu, qui enlèves le péché du monde, donne-nous la paix.

COMMUNION

Ref : Ndiyo sasa tumpokee Mungu Mwana katika mkate mweupe, bora na safi. Akaamo pasipo kuonekana, Ajificha, ni fumbo lake mwenyezi.

Kwa woga wetu amejificha humo, ndiyo maana hatuoni sura yake. Twampokea kama waana vipofu na kula mwili wake katika Hostia.

Mkate huo, ndiyo mwili wake Mungu, na divai ndiyo damu yake safi. Vyote vyafanyiwa katika Umungu, ni mujiza mkubwa kwa sisi vipofu.

POSTCOMMUNIO

Ref: Wewe, baba Domingo, tunakuomba, utuombee, tunakuomba, utulinde. (bis)

Baba, baba, tunza wito wetu, Mtume wa wito, tunza wito wetu. (bis)

1. Mavuno ni mengi, ee Baba, Lakini wafanya kazi ni wachache. (bis)

Baba, baba, tunza wito wetu, Mtume wa wito, tunza wito wetu. (bis)

2. Mwombeni Bwana wa mavuno, atume wafanya kazi mu mavuno. (bis)

Baba, baba, tunza wito wetu, Mtume wa wito, tunza wito wetu. (bis)

SORTIE

Ref :Nitamwimbia Bwana wangu sifa siku zote za maisha yangu, nitamwimbia. kwani yeye ni mwema sana,. ndiyo maana nitamwimbia sifa yade (2x)

  1. Ee moyo wangu, umsifu Bwana, Yeye ni mwema, jina lake takatifu (2).

  2. Baba wa mbingu, ulinipa uzima, vyote kwa wema.

  3. Bwana wa mbingu ulinipa akili, vyote kwa wema.